Maimbodo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Maimbodo (kwa Kifaransa: Maimboeuf; alifariki Dampierre, karibu na Besançon, Burgundy, katika Ufaransa wa leo, karne ya 9 hivi) alikuwa Mkristo mkaapweke wa Ireland aliyekwenda kuhiji patakatifu mbalimbali pa barani Ulaya hadi alipouawa na majambazi[1][2][3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu. Papa Leo XIII alithibitisha heshima hiyo tarehe 24 Novemba 1900[4].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Januari[5].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads