Maliki Junubi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Maliki Junubi (ing. na lat. Regulus pia α Alfa Leonis, kifupi Alfa Leo, α Leo) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Simba (pia Asadi, lat. Leo).

Remove ads
Jina
Maliki Junubi inayomaanisha “Mfalme wa Kusini” ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [1]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema المليك al-malik linalomaanisha "mfalme". Waarabu waliwafuata hapa Wagiriki wa Kale waliosema βασιλίσκος basiliskos (mfalme mdogo). Jina mbadala lilikuwa “moyo wa simba” yaani قلب الأسد qalb al-asad. Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali umbo la Kilatini la jina na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Regulus" [2] (yaani mfalme mdogo).
Alfa Leonis ni jina la Bayer maana ina nafasi ya kwanza kufuatana na mwangaza katika kundinyota yake.
Remove ads
Tabia
Maliki Junubi - Regulus iko umbali wa miakanuru 77.5 kutoka Jua letu. Ina mwangaza unaoonekana wa 1.36 na mwangaza halisi ni -0.2. Spektra yake ni ya aina ya B7.
Iko angani karibu na mstari wa ekliptiki, hivyo inafunikwa mara nyingi na Mwezi.
Maliki Junubi ni mfumo wa nyota maradufu nne au labda zaidi. Nyota kuu ni Regulus A iliyo na rangi ya buluu-nyeupe na masi ya 3.5 Inafuatana na nyota kibete nyeupe yenye masi ya M☉ 0.3 na zote mbili zinazunguka kwa pamoja kitovu chao cha graviti katika muda wa takriban siku 40.[3].
Nyota mbili nyingine ya mfumo huu zinaitwa B na C zikiwa umbali wa vizio astronomia 5,000 kutoka A.
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya Nje
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads