Margareta wa Uskoti
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Margareta wa Uskoti (1046 – 1093) alikuwa malkia wa Uskoti kama mke wa mfalme Malkolm III.

Mwaka 1250 ametangazwa na Papa Innocent IV kuwa mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 16 Novemba[1].
Maisha
Margareta alizaliwa mwaka 1046 nchini Hungaria, ambako baba yake aliishi uhamishoni.
Aliolewa na Malkolm III, mfalme wa Uskoti, akapata watoto wanane.
Alikuwa mfano wa pekee kama mke bora, mama halisi na malkia wa nchi, akijitahidi sana kuistawisha pamoja na Kanisa, akiunganisha na sala na saumu ukarimu kwa maskini [2].
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads