Matt Damon

From Wikipedia, the free encyclopedia

Matt Damon
Remove ads

Matthew Paige Damon (amezaliwa tar. 8 Oktoba 1970) ni mwigizaji wa filamu na mhisani kutoka nchini Marekani. Ameshinda Tuzo ya Akademi akiwa kama mwandishi bora muswaada andishi kwa filamu ya Good Will Hunting, ana tunukiwa unyota bora kwa filamu hiyohiyo.

Ukweli wa haraka Amezaliwa, Kazi yake ...

Umaarufu wake ulianza kukua katika soko la filamu kuanzia mwaka wa 1997, tangu hapo akawa ana pambanishwa na waigizaji wakubwa-wakubwa wa wa A-list, na leo hii ni mmoja kati ya waigizaji wakubwa kabisa katika Hollywood.

Damon amepata kushiriki katika baadhi ya filamu maarufu kama vile Saving Private Ryan, The Talented Mr. Ripley, mfululizo wa Ocean, mfululizo wa Bourne, Syriana, The Good Shepherd na The Departed. Amejishindia Matuzo kedekede kwa umahili wake wa uigziaji wa filamu na amepokea nyota katika Hollywood Walk of Fame.

Damon ni mmoja kati ya wale waigizaji ishirini na tano bora kwa muda wote. Katika mwaka wa 2007, alipewa jina na gazeti la People kuwa yeye ni Mwanaume Mwenye Mvuto Aliye Hai.

Damon amekuwa akijishughulisha na kazi za kihisani mara kwa mara, kazi hizo ni pamoja na lujitolea kwa ONE Campaign na H2O Africa Foundation. Pamoja akiwa na mke wake, Bi. Luciana Bozán Barroso, Damon amepata watoto wawili wa kike, mmoja anaitwa Isabella na mwingine anaitwa Gia, na pia ana mtoto wa kufkia Alexa kutoka katika ndoa ya awali aliyofunga Bi. Barroso.

Remove ads

Filamu

Maelezo zaidi Mwaka, Filamu ...
Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads