Matthew Ayariga
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Matthew Ayariga alikuwa Mkristo kutoka Ghana[1][2][3][4][5][6][7] ambaye, pamoja na Wakopti 20 kutoka Misri[8], alitekwa na Waislamu wenye itikadi kali wa Daish huko Sirte, Libya, alipokuwa anafanya kazi ya ujenzi mnamo 27 Desemba 2014 au Januari 2015.[9]
Hatimaye waliuawa wote pamoja kwa kukatwa kichwa kwa ajili ya imani yao[10][11][12][13][14], kama ilivyoonyeshwa katika video tarehe 15 Februari 2015[15]. Kifo chao kilithibishwa na serikali na Kanisa[16].
Tarehe 21 Februari 2015 Patriarki Tawadros II wa Alexandria aliwatangaza kuwa watakatifu[17]. [17]. Kwa ruhusa yake, Papa Fransisko aliwaingiza katika Martyrologium Romanum.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe ya kifodini chao, 15 Februari.
Remove ads
Marejeo
Martin Mosebach aliandika kitabu juu yao: The 21 - A Journey into the Land of Coptic Martyrs.[18]
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads