Mbarali

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mbarali
Remove ads

Wilaya ya Mbarali ni wilaya mojawapo kati ya 7 za Mkoa wa Mbeya. Wilaya hiyo ilianzishwa mnamo mwaka 2000.

Thumb
Mahali pa Mbarali (kijani cheusi) katika mkoa wa Mbeya.

Upande wa Kaskazini Mashariki inapakana na Wilaya ya Iringa Vijijini, upande wa Mashariki inapakana na Wilaya ya Njombe, upande wa Kusini inapakana na wilaya ya Mbeya na Kaskazini na Wilaya ya Chunya.

Wakazi

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 234,908 [1]. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 446,336 [2].

Makabila makuu yaliyopo wilayani Mbarali ni Wasangu, Wahehe, Wakinga, Wabena na Wanyakyusa. Vilevile yapo makundi madogo ya makabila kama Wasukuma, Wawanji, Wabarbaig na Wagogo.

Makundi mengi ya makabila haya ni wakulima na wafugaji ambao walihamia bonde la Usangu kutoka Mikoa ya Arusha, Mwanza, Shinyanga, Singida na Dodoma.

Remove ads

Eneo

Eneo lake ni kilometa za mraba 16,000. Katika eneo hili ardhi kwa ajili ya kilimo ni asilimia 20, eneo la wanyama pori takriban 30 %, hifadhi za misitu 1%, maeneo ya makazi mnamo 38% na maeneo ya pori tariban 16%.

Wilaya ya Mbarali iko hasa tambarare ya chini katika Bonde la Ufa. Maji hutelemka kutoka milima na mitelemko ya kando na kukusanyika hapa hivyo wilaya ni a chanzo kikuu cha maji ambacho ni mto Ruaha Mkuu na kuelekea mto Rufiji, halafu Bahari Hindi.

Remove ads

Ekolojia

Kunda kanda tatu za kiekolojia ambazo ni:

  • Uwanda wa Msangaji katika kaskazini una udongo mwenye rutba kidogo, unapokea mvua mm 500 - 900 kwa mwaka na ni sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
  • Uwanda wa kati wa Usangu una udongo mweusi na kichanga, unapokea mvua mm 450-650 kwa mwaka ukitumiwa kwa kilimo cha mtama, uwele, mahindi, mpunga na kwa ufugaji.
  • Tambarare za Kusini mwa Usangu. Hapa mvua ni haba, mm 360-750. Kilimo ni cha mahindi, karanga, pamba, kilimo cha umwagiliaji cha mpunga halafu ufugaji.

Tanbihi

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads