Pamba

From Wikipedia, the free encyclopedia

Pamba
Remove ads
Remove ads

Pamba ni nyuzi nyeupe na laini zinazotokana na tunda la mpamba (Gossypium sp.). Nyuzi hizi zinaonekana kama sufi na mipamba inalimwa kwa nyuzi hizi ambazo ni msingi wa kutengeneza kitambaa na nguo.

Kwa matumizi mbalimbali ya neno hili angalia hapa


Thumb
Pamba tayari kwa mavuno

Ndani ya tunda nyuzi za pamba zinaunganishwa na punje za mbegu wa mmea. Kusudi yao ni kusambaza mbegu kwa sababu zinafanya kazi kama tanga zinashika nguvu ya upepo na kuwezesha mbegu kuelea hewani mbali kiasi.

Pamba yenyewe inapatikana kutoka spihi nyingi za gossypium zinazokua kiasili katika sehemu mbalimbali za dunia. Lakini karibu pamba yote inayolimwa kwa matumizi ya nguo imetokana na spishi nne za mipamba ambazo ni

  • Gossypium herbaceum L. (asili ya Asia)
  • Gossypium arboreum L. (asili ya Asia)
  • Gossypium hirsutum L. (asili ya Amerika)
  • Gossypium barbadense L. (asili ya Amerika).

Kitambaa cha pamba huwa na faida nyingi kuliko vitambaa vya sintetiki. Pamba inaweza kushika unyevu hadi asilimia 80% ya uzito wake hivyo kitambaa chake kinapendeza hasa katika mazingira ya joto kwa sababu mtu husumbuliwi sana na jasho.

Thumb
Mipamba shambani
Thumb
Fukusitunda (Anthonomus grandis) anakula mpamba na kutaga mayai ndani ya matunda yake na kuharibu mavuno
Thumb
Mavuno ya kisasa kwa kutumia mashine inayovuna pamba na kuigandamiza kama mabloku makubwa kwa usafiri
Remove ads

Mavuno duniani 2004/2005

2004/2005 jumla ya tani 26.043.000 t za pamba zilivunwa duniani. Nchi zenye mavuno kubwa zilikuwa zifuatazo:

Maelezo zaidi Rang, Nchi ...
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pamba kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads