Ukoo

kundi la watu wamoja na ujamaa halisi From Wikipedia, the free encyclopedia

Ukoo
Remove ads
Remove ads

Ukoo ni chanzo na muunganiko wa familia kadhaa zenye asili moja[1]. Mara nyingi huwa na utamaduni na lugha moja. Ukoo huundwa na vizazi mbalimbali ambapo mila na desturi zao huendelezwa na kuhifadhiwa kwa faida ya vizazi vya baadae. Mfano mmojawapo ni ukoo wa Mkwawa uitwao ukoo wa Mwamuyinga.

Thumb
Ukoo wa Wahehe mkoani Iringa mwanzoni mwa karne ya 20.

Katika eneo la Maziwa Makuu ya Afrika, ukoo ni kitengo cha shirika la kijamii. Ni muundo wa zamani sana wa jamii katika eneo hilo, zaidi ya familia na kizazi. Muundo huo unapatikana katika Rwanda ya sasa, Burundi, Tanzania na Uganda.

Watu wa eneo hilo hutumia maneno tofautitofauti ya kiasili kuelezea dhana hiyo: ubwoko nchini Rwanda, umuryango nchini Burundi, ruganda katika falme za Bunyoro na Buhaya, igise huko Buha, ishanja huko Buhavu na ebika huko Buganda.

Uanachama wa ukoo ni dhana huru, yenye uwiano na nasaba, iliyojikita zaidi katika utamaduni na imani binafsi kuliko ushahidi halisi.

Remove ads

Marejeo

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads