Meitneri

From Wikipedia, the free encyclopedia

Meitneri
Remove ads

Meitneri (meitnerium) ni elementi ya kikemia yenye alama ya Mt na namba atomia 109. Ni elementi sintetiki nururifu ambayo haipatikani kiasili lakini inaweza kuundwa katika maabara. Isotopi yake thabiti zaidi ni meitneri-278 iliyo na nusumaisha ya sekunde 4.5.


Ukweli wa haraka Meitneri (Meitnerium) ...
Remove ads

Ilitegenezwa mara ya kwanza kwenye mwaka 1982 katika maabara ya taasisi ya utafiti wa ioni nzito ya GSI Helmholtz huko Darmstadt, Ujerumani.[1]

Imepokea jina lake kwa heshima ya mwanafizikia wa kike wa Ujerumani Lise Meitner .

Thumb
Meitnerium ilipewa jina la mwanafizikia Lise Meitner, mmoja wa wavumbuzi wa mwatuko nyuklia.

Wavumbuzi walifyatua viini vya chuma-58 kwa bismuthi-209 wakagundua atomu moja pekee ya isotopi meitneri-266:[2]

Uvumbuzi huu ulithibitishwa miaka mitatu baadaye huko Dubna (Umoja wa Kisovyeti).[2]

Hakuna habari kuhusu tabia za kikemia za Meitneri maana inaweza kutengenezwa tu kwenye maabara kwa viwango vidogo sana lakini kwa gharama kubwa, na baada ya kutengenezwa haidumu, maana atomu zake zinaachana haraka katika muda wa sekunde kadhaa.

Remove ads

Marejeo

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads