Miguel de Cervantes

From Wikipedia, the free encyclopedia

Miguel de Cervantes
Remove ads

Miguel de Cervantes Saavedra (29 Septemba 154723 Aprili 1616) alikuwa mwandishi wa Hispania anayesifiwa kama mwandishi bora kabisa wa nchi yake. Mara nyingi riwaya yake "Don Quixote" [1] inahesabiwa kati ya vitabu muhimu zaidi vya fasihi ya Ulaya nzima. Riwaya hii imetafsiriwa kwenda lugha zaidi ya 140 na kuifanya kuwa kitabu kilichotafsiriwa kwa lugha nyingi zaidi duniani baada ya Biblia.

Thumb
Cervantes alivyochorwa.
Remove ads

Maisha

Cervantes alizaliwa kama mtoto wa nne kati ya saba wa mganga. Hakuna habari kamili juu ya maisha yake kama kijana.

Alipokuwa na miaka 23 alijiunga na jeshi la wanamaji wa Hispania akashiriki kwenye mapigano ya Lepanto dhidi ya milki ya Osmani alipojeruhiwa na kupotewa na mkono wa kulia.

Mwaka 1575 alikamatwa na maharamia Waalgeria akawa mfungwa hadi kununuliwa na wamonaki Wakristo waliomrudisha nyumbani.

Tangu mwaka 1584 alianza kuandika lakini mwanzoni bila mafanikio ya kipesa. Alipata kazi kama mkusanyaji kodi lakini alishindwa kuonyesha hesabu safi ya mikusanyo yake akatupwa jela. Hapo alianza kazi ya kuandika riwaya yake ya "El ingenioso Hidalgo Don Quijote de la Mancha" iliyotolewa mwaka 1605 na sehemu ya pili ikafuata mwaka 1615.

Hata hivyo alikufa maskini na sifa zake zilikua baada ya kifo chake tu.

Upande wa dini, alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki. Mwaka 1613 alijiunga na Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko na tarehe 2 Aprili, siku kadhaa kabla ya kifo chake, aliweka nadhiri yake kamili.[2]

Remove ads

Kazi

  • El ingenioso hidalgo Don Quixote de la Mancha (1605): First volume of Don Quixote.
  • Novelas ejemplares (1613): mkusanyiko wa hadithi fupi 12:
    • "La gitanilla" ("The Gypsy Girl")
    • "El amante liberal" ("The Generous Lover")
    • "Rinconete y Cortadillo" ("Rinconete & Cortadillo")
    • "La española inglesa" ("The English Spanish Lady")
    • "El licenciado Vidriera" ("The Lawyer of Glass")
    • "La fuerza de la sangre" ("The Power of Blood")
    • "El celoso extremeño" ("The Jealous Man From Extremadura")
    • "La ilustre fregona" ("The Illustrious Kitchen-Maid")
    • "Novela de las dos doncellas" ("The Novel of the Two Damsels")
    • "Novela de la señora Cornelia" ("The Novel of Lady Cornelia")
    • "Novela del casamiento engañoso" ("The Novel of the Deceitful Marriage")
    • "El coloquio de los perros" ("The Dialogue of the Dogs")
  • Segunda Parte del Ingenioso Cavallero [sic] Don Quixote de la Mancha (1615): Second volume of Don Quixote.
  • Los trabajos de Persiles y Sigismunda (1617).
  • La Galatea
Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads