Akili ya binadamu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Akili ya binadamu (kwa Kiingereza "mind"[3]) ni kipawa kinachowezesha kufikiri, kuelewa, kuwasiliana, kujifunza, kupanga na kutatua matatizo. Ni ufahamu unaotumia ubongo na unaomwezesha binadamu hata kutofautisha jambo kwa wema na ubaya wake upande wa maadili na hatimaye kumuongoza katika kufanya maamuzi kwa kutumia hiari yake[4].


Dhana kuhusu asili ya akili ya binadamu zinatofautiana, vilevile na maelezo mengine mengi, kulingana na dini, falsafa na sayansi[5] husika.
Jambo mojawapo la msingi ni kuelewa kama akili hiyo ya pekee inategemea tu ubongo uliokua sana katika binadamu kuliko katika spishi nyingine au kuna athari kubwa ya roho ndani yake. Hii ni kwa sababu walichoweza kufanya watu hakifanani kabisa na wanyama walichofanya, hata wale walio na ujirani naye kibiolojia kama sokwe.
Remove ads
Tazama pia
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads