Mitumba

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Mitumba ni neno la Kiswahili, ambalo maana yake halisi ni "vifurushi", na linalotumiwa kurejelea vifurushi vilivyofungwa vya plastiki vya nguo zilizotolewa na watu katika nchi tajiri. Neno hili pia linatumika katika mavazi ambayo hufika kwenye vifurushi hivyo.

Moja ya bandari kuu inayopokea mitumba ipo nchini Tanzania jiji la Dar es Salaam. Kutoka hapo mavazi yanatawanywa ndani ya bara la Afrika.

Usafirishaji na uuzaji wa mitumba unafanyika kwa namna nyingi katika kampuni tajiri na katika nchi za Afrika ambapo mitumba inanunuliwa na kuuzwa.

Wakosoaji wa biashara ya mitumba wanaona kuwa uwepo wa nguo za bei nafuu unachangia kudorora kwa viwanda vya nguo vya ndani. [1]

Wafuasi wa mitumba wanaeleza kuwa mavazi hayo yana manufaa kwa kuwa yanachochea shughuli za kiuchumi na kuwaruhusu watu wenye uwezo mdogo kumudu mavazi ya mtindo. [2]

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads