Mkoa wa Kidal

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mkoa wa Kidal
Remove ads

Mkoa wa Kidal (kwa Kibambara: Kidal Dineja) ni eneo la utawala nchini Mali. Mkoa huo una eneo la kilomita za mraba 151,450. Wakati wa sensa ya mwaka 2009 walikuwepo wakazi 67,638 [1].

Thumb
Eneo la Mkoa wa Kidal
Thumb
Ranabi ya Nkoa wa Kidal (pamoja na Mkoa wa Gao)

Eneo hili hapo awali lilikuwa sehemu ya Mkoa wa Gao, lakini lilitengwa kama mkoa wa pekee mnamo 1991. Mkoa uko kwenye kaskazini ya Mali. Makao makuu ya utawala wa mkoa yako Kidal mjini.

Remove ads

Jiografia

Mkoa huu umepakana na Mkoa wa Timbuktu upande wa magharibi, Mkoa wa Gao upande wa kusini, nchi ya Niger upande wa mashariki na Algeria upande wa kaskazini.

Kidal ina tabianchi ya jangwa na halijoto ya mchana inaweza kufikia nyuzi 45°C.

Miji mikubwa zaidi ya eneo hilo ni Kidal, Tessalit na Aguel'hoc .

Usafiri na uchumi

Biashara kuu ya Mkoa wa Kidal ni pamoja na ufugaji na biashara. Kilimo cha kibiashara kimeendelezwa katika baadhi ya sehemu. Eneo hilo ni vigumu kufikia, hakuna barabara kuu za lami au mito ya usafirishaji.

Historia

Kidal iliona maasi ya Watuareg kwenye miaka 1963–1964 na 1990–1991. Makubaliano ya Tamanresset yalifuata Januari 6, 1991, na kuunda Mkoa wa Kidal mnamo 8 Agosti 1991. Katika mapigano hayo, idadi kubwa ya wakazi, hasa Watuareg na Wasonghai walikimbia hadi Afrika Kaskazini katika miaka ya 1990.

Mwishoni mwa 2011, kundi nyingine la waasi wa Watuareg, Harakati kwa Ukombozi wa Azawad (MNLA), lilitokea katika eneo hilo. [2] Harakati ilitangaza kaszaini yote ya Mali kuwa jamhuri huru ya Azawad mnamo Aprili 2012 ambayo haikutambuliwa kimataifa.

Lakini baada ya wiki chache, wanamgambo Waislamu walishinda MNLA na kuchukua utawala mkononi mwao. Jeshi la Kifaransa lilifika kufuatana na maombi ya serikali ya Mali na kuwaondoa wanamigambo hao hadi Januari 2013. [3]

Utamaduni

Eneo hili linakaliwa na Watuareg ambao ni kabila la kuhamahama lenye asili ya Waberberi. Uandishi wao ni alfabeti Tifinagh.

Wilaya

Thumb
Wilaya za Mkoa wa Kidal

Mkoa wa Kidal umegawanywa kwa wilaya (cercles) nne: [4]

Maelezo zaidi Jina la Cercle, Eneo (km2) ...

Angalia pia

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads