Mlima Meru

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mlima Meru

Mlima Meru ni mlima wenye asili ya volkeno na urefu wa mita 4566 (futi 14980) juu ya usawa wa bahari. Mlima huo ni wa tano kwa urefu katika bara la Afrika.

Thumb
Mlima Meru, mwaka 2012.
Thumb
Mlima Meru kutoka juu.
Thumb
Kilele cha Mlima Meru.

Mlima katika hifadhi ya taifa

Mlima Meru unapatikana ndani ya Hifadhi ya Arusha ambayo ilianzishwa mwaka 1960 na ambapo wanyamapori kuzunguka Maziwa ya Momella na volkeno ya Ngurudoto (Ngurudoto crater) walihifadhiwa na kulindwa katika eneo hili.

Hifadhi hiyo ina ukubwa wa kilometa za mraba 137 na ipo umbali wa kilometa 35 kutoka mji wa kitalii wa Arusha na Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro.

Jina la mlima huu limetokana na kabila maarufu nchini Tanzania la Wameru ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi na kuuzunguka mlima huu.

Vivutio katika hifadhi hiyo vinajumuisha volkeno, maziwa, misitu na wanyamapori kama twiga, tembo, pundamilia, nyati na wengine wengi. Pia kuna ndege wa aina nyingi wakiwemo flamingo, na misitu katika mlima Meru ni makazi ya nyani.

Kupanda Mlima Meru kunachukua siku tatu hadi nne na wakati mzuri kwa kupanda mlima ni kuanzia mwezi Juni hadi Februari ambapo mvua zinaweza kunyesha katika mwezi Novemba. Na wakati mzuri wa kuona mlima Kilimanjaro kutokea Meru ni kati ya Desemba na Februari.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Picha

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.