Walowezi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Walowezi (kutoka kitenzi "kulowea"; pia: setla, kutoka Kiingereza "settler") ni watu ambao wamehamia katika eneo fulani na kuanzisha makazi ya kudumu pale, hata mara nyingi kulitwaa eneo hilo. Makazi mara nyingi hujengwa kwenye ardhi ambayo inadaiwa au inayomilikiwa na watu wengine.

Wao wenyewe wakati mwingine huondoka katika kujitafutia riziki au uhuru wa dini[1].
Mara nyingine walowezi huungwa mkono na serikali au nchi kubwa au tajiri[2].
Remove ads
Sababu za uhamiaji
Sababu za kuhama kwa walowezi hutofautiana, lakini mara nyingi huwa ni mambo yafuatayo: hamu ya mwanzo mpya na maisha bora katika nchi ya kigeni, hali duni ya kifedha, dhuluma ya kidini[1], ya kijamii, ya kiutamaduni au ya kikabila[2], kukandamizwa kisiasa, na sera kutoka serikali zinazowapa motisha wananchi kwa lengo la kuhamasisha makazi ya kigeni.[3]
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads