Filomena wa Roma

From Wikipedia, the free encyclopedia

Filomena wa Roma
Remove ads

Filomena wa Roma (10 Januari 291 - 10 Agosti 304) alikuwa bikira wa ukoo tawala wa Corfu (Ugiriki) ambaye alianza kuheshimika kama mtakatifu mfiadini baada ya masalia kupatikana mnamo Mei 1802 katika katakombu ya Priscilla, Roma, Italia. Paliandikwa Pax Tecum Filumena (yaani "Amani kwako, Filomena"). Kabla ya hapo hakujulikana, lakini baadaye heshima ya Wakatoliki na Waorthodoksi wengi kwake imestawi sana hadi leo sehemu nyingi za dunia ikisaidiwa na njozi na miujiza iliyotokea kwa kuomba sala zake.

Thumb
Mt. Filomena katika kanisa kuu la Montauban.
Thumb
Sanamu ya Mt. Filomena, kazi ya Johann Dominik Mahlknecht, Museum Gherdëina, huko Urtijëi, Italia.

Kati ya miaka 1837 na 1961 Kanisa Katoliki liliruhusu heshima hiyo katika liturujia pia.[1] Lakini wasiwasi wa wanahistoria umefanya jina lake liondolewe katika kalenda zote za watakatifu.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads