Mti wa uzima
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mti wa uzima (kwa Kiebrania עֵץ הַֽחַיִּים, Etz haChayim,) ni mfano unaotumiwa na Biblia.[1]

Katika kitabu cha Mwanzo, mti wa uzima unapatikana katika mstari 2:9 kama mti uliopandwa na YHWH Elohim (יְהוָה אֱלֹהִים) karibu na mti wa ujuzi wa mema na mabaya (עֵץ הַדַּעַת) "katikati ya bustani ya Eden".[2]
Katika 3:24 imeandikwa kwamba baada ya dhambi ya asili kerubi analinda njia inayofikia mti wa uzima.
Kitabu cha Mithali kinatumia jina hilo mara nne (3:18, 11:30, 13:12 na 15:4).
Hatimaye Kitabu cha Ufunuo kinatumia usemi wa Kigiriki ξύλον (τῆς) ζωής, xylon (tēs) zōës, mara nne vilevile (2:7, 22:2, 22:14 na 22:19.

Kwa kawaida Wakristo wamechukua usemi huu kama wa fumbo kwa msalaba wa Yesu.
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads