Kerubi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kerubi
Remove ads

Kerubi (kutoka Kiebrania כְּרוּב, kərūv, wingi כְּרוּבִים, kərūvîm[1]) ni kati ya viumbe visivyoonekana wanaotajwa na Biblia. Ndiyo sababu wakaja kujumlishwa kati ya malaika[2], ingawa Agano la Kale halisemi hivi wazi[3].

Thumb
Kerubi mwenye mabawa sita alivyochorwa na Wakristo.
Thumb
James Tissot - Sanduku la Agano likivuka Yordani.

Asili yake ni katika visasili vya historia ya awali, hasa vya Mesopotamia.

Ingawa Amri kumi za Mungu kwa Musa zimekataza sanamu (Kut 20), kurasa chache mbele (Kut 25) Mungu alimuagiza azitengeneze mbili za makerubi na kuziunganisha na kifuniko cha sanduku la Agano ambamo hizo amri zilitunzwa. Pia sura zao zipatikane katika mapazia ya kandokando.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads