Mto Bloukrans (KwaZulu-Natal)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mto Bloukrans (KwaZulu-Natal) unaanzia Emangosini Njesuthi Drakensberg, eneo la KwaZulu-Natal, Afrika Kusini. Unaendelea upande wa kaskazini magharibi, unapita kijiji cha Frere, kisha unaungana na mto Tugela.

Mto na matawimto yake havina mabwawa, ingawa umwagiliaji unatokea katika maeneo ya juu.
Jina lina asili katika Kiholanzi "Blaauwekrans" (Kizulu: Msuluzi) kutokana na miamba yenye rangi ya buluu katika eneo hilo.[1]
Tawimto kubwa la Bloukrans ni mto Nyandu ambao una tawi la Sterkspruit. Matawi mengine ni mito midogo ya Ududuma, Umsobotshe na Ubhubhu.
Shamba la De Hoek linapatikana sehemu ya juu ya Bloukrans.
Remove ads
Tazama pia
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads