Rhine
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Rhine (tamka: rain) (kwa Kijerumani Rhein, Kifaransa Rhin na Kiholanzi Rijn) ni kati ya mito mirefu ya Ulaya.
Remove ads
Chanzo na nchi inapopita

Ina chanzo chake katika milima ya Uswisi. Inapita katika Uswisi, Ujerumani na Uholanzi; mwendo wake ni pia mpaka kati ya Uswisi na Liechtenstein, Uswisi na Austria halafu Ujerumani na Ufaransa.
Mpakani kati ya Uswisi na Ujerumani mto inapita katika ziwa la Konstanz (au: Bodensee).
Njia ya maji
Kuanzia mji wa Rheinfelden hadi Rotterdam kwa urefu wa zaidi ya 800 km mto unapitika kwa meli za mtoni.
Usafiri mtoni ni muhimu kwa ajili ya viwanda vingi vilivyopo kando la mto.
Kihistoria Rhine pamoja na mto Danubi ilikuwa mpaka wa kakazini ya Dola la Roma.
Delta ya Rhine
Ndani ya Uholanzi mto hujigawa kuwa na mikono mikubwa miwili inayoitwa Waal na Lek. Mbele ya mji wa Rotterdam inaungana tena kuwa mto mmoja.
- Rhine inayoingia katika ziwa la Konstanz
- Maporomoko ya Rhine kwa Schaffhausen
- Mdomo wa Rhine karibu na Rotterdam
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Rhine kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads