Senegal (mto)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mto wa Senegal ni kati ya mito mirefu ya Afrika ukiwa na urefu wa kilometa 2272 pamoja na tawimto mrefu la Bafing.
Remove ads
Mto Senegal wenyewe unaanza karibu na mji wa Bafoulabe (Mali) kwenye maungano ya mito miwili ya Bafing na Bakoye ambayo yote ina chanzo huko Guinea.
Urefu wa mto Senegal ni mpaka kati ya Mauretania na Senegal. Senegal ikikaribia bahari ya Atlantiki inafika kwenye kisiwa cha St. Louis halafu inageukia kusini. Sasa inafuata pwani ya bahari ikitengwa na Atlantiki kwa kanda nyembamba ya mchanga tu hadi kuingia bahari ya Atlantiki.
Beseni la Senegal ni kilometa za mraba 483,181. Matawimto muhimu ni mto Faleme, mto Karakoro na mto Gorgol.
Mali, Mauritania, Senegal na Guinea zimeshirikiana katika mamlaka ya beseni la mto wa Senegal (Organisation pour la mise en valeur du fleuve Sénégal - OMVS).

Remove ads
Tazama pia
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Senegal (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads