My Life
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
"My Life" ni kibao cha tatu cha rapa The Game kutoka katika albamu yake ya tatu, LAX ambao ilitolewa mnamo tar. 22 Agosti 2008. Wimbo umetayarishwa na Cool na Dre, ukimshirikisha Lil Wayne, na ipo kama jinsi nyimbo zake nyingi za karibuni alizotoa Lil Wayne, anatumia kionjo cha Auto-Tune kwa ajili ya kiitikio.
Remove ads
Historia
Kurekodi
Watayarishaji Cool na Dre wametoa makala ya video yanayoonyesha namna walivyotengeneza biti la wimbo huu.[2]
The Game alizungumza juu ya kazi yake waliyofanya na Lil Wayne na kueleza:
Unapokuwa ndani ya studio na Wayne, unaweza kutulia sana yaani, mshikaji, kwa sababu kila kitu kina kuwa rahisi kinoma. Anaweza kwenda na mamelodi ajabu. Pindi apigapo na ma-idea, au niibuke na ma-idea, tunanyoosha, mwana. Mchakato wake ni rahisi. Ninafikiri mimi na yeye labda tungeweza kufanya albamu, kama, sikui saba hivi. Albamu bab-kubwa! Anaiwekea 100, naiwekea 100. Sote ni Ma-MC wenye vipaji. Nakumbali sana kwenye hip-hop.[3]
Remove ads
Nafasi ya chati
"My Life" ilitolewa kwa mara ya kwanza kupiti maduka ya iTunes huko Amerika ya Kaskazini kwa ajili upakuaji wa dijitali. Nchini Marekani, iliingia kwa kushika nafasi ya #21 kwenye chati za Billboard Hot 100 inaifanya kuwa kibao pekee cha The Game kushika nafasi ya juu sana kwenye chati. Pia iliingia na kushika nafasi ya #32 kwenye Pop 100 ambayo pia inashughulika na masuala ya upakuaji mkondoni. Huko nchini Kanada iliingia na kushika nafasi ya #42 kwenye chati za Canadian Hot 100 na wiki hiyohiyo pia ikaingizwa kwenye orodha upakuaji mkondoni. Kwenye chati za UK Singles Chart ma kushika nafasi ya #34.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads