Lil Wayne

From Wikipedia, the free encyclopedia

Lil Wayne
Remove ads

Dwayne Michael Carter, Jr. (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Lil Wayne; amezaliwa 27 Septemba 1982) ni mshindi wa Tuzo za Grammy - akiwa kama rapa wa muziki wa hip hop bora kutoka nchini Marekani.

Ukweli wa haraka Maelezo ya awali, Amezaliwa ...

Alijiunga na studio ya Cash Money Records akiwa bado yungali bwana mdogo na akabahatika kufanya rekodi kadhaa katika studio hiyo. Wayne alikuwa mmoja kati ya waliokuwa wanachama wa kikundi cha muziki wa rap cha Hot Boys.

Remove ads

Waasifu

Maisha ya awali

Alizaliwa kama Dwayne Michael Carter, Jr. na kukulia mjini Hollygrove karibu kidogo na mji wa New Orleans, Louisiana. Akiwa na umri wa miaka kumi na moja, akakutana na Bryan Williams, rapa na ndiyo mmiliki wa studio ya Cash Money Records.

Baada ya makutano hayo, Wayne akarekodi rap flani ya michano katika studio hiyo ya Williams kwa kutumia chombo maalum cha kuweza kukujibu wakati unachana. Na kwa bahati nzuri michano hiyo ilimwacha hoi mmiliki huyo wa studio na kuthubutu hata kumwingiza Wayne katika studio yake.

Wayne pia ana mtoto wa kike mmoja aitwaye Reginae Carter, aliyezaliana na Antonia "Toya" Johnson, mpenzi wake wa kitambo toka shule. Wawili hao walikuja kuoana wakati wa Siku Kuu ya Wapendanao ya mwaka wa 2004, lakini walikuja kutalikiana mnamo mwaka wa 2006.

Remove ads

Muziki

Albamu za Lil Wayne

  • 1999: Tha Block Is Hot
  • 2000: Lights Out
  • 2002: 500 Degreez
  • 2004: Tha Carter
  • 2005: Tha Carter II
  • 2008: Tha Carter III
EP albums
  • 2007: The Leak

Filamu

  • Baller Blockin (2000)
  • Who's Your Caddy? (2007)
  • Fast and Furious (2009) (inakuja)
  • The Boondocks in the "Invasion of the Katrinians" sehemu ya [1] (2007)
  • "Access Granted" (2007) [2]
  • Hurricane Season (inakuja)[3]
  • Lil Wayne Documentary (2009) (inakuja)[4]

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads