Nameless

Mwimbaji kutoka nchini Kenya From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

David Mathenge (amezaliwa Agosti 1976), anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii Nameless, ni msanii wa kapuka nchini Kenya.

Taawasifu

Yeye alipata umaarufu mwaka 1999 kupitia Ushindani wa "Star search" uliofanywa na stesheni ya radio ya [Capital(98.4 fm) http://www.capitalfm.co.ke], ambayo alishinda kwa wimbo wake wa awali "Megarider" Wimbo huu unaongelea m kijana ambaye hana pesa na ilhali anajaribu kumpata kipusa.Fedha alizonazo zinatosha tu tiketi ya Kenya Bus , na si maisha ambayo msichana huyo anataka. Alifanya wimbo huo na na mtayarishaji Tedd Josiah na ulikaa kwenya kwenye chati kwa wiki kadhaa Alitia saini na Ogopa Deejays mnamo mwaka wa 2001.katika Ogopa DJ's alikuwa pamoja na wasanii kama vile marehemu E-Sir amabaye walifanya wimbo wa "Boomba Train," na Amani : "Ninanoki" mwaka wa 2002 wimbo ambao ulivunja rekodi kwenya chati nchini Kenya kwa kusalia siku 110 nambari moja

Amekwenda kwenye ziara kaadhaa Afrika Mashariki , Marekani na pia Uingereza Alitoa albamu yake ya "on fire mwaka wa"2004. Pia mwaka huo huo wa 2004 Mathenge alimuoa msanii mwenzake Wahu Kagwe waliyekuwa wakirekodi pamoja katika Ogopa DJ's. Wana mtoto mmoja, binti ambaye alizaliwa mwaka 2006. Yeye pia ni mbunifu na alfuzu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.

Kikundi cha 'pop' kutoka Afrika Kusini ; Jamali walitoa wimbon wimbo wa "nigger" na ilisemekana kwamba waliuiba wimbo huo kutoka kwa Nameless. Lakini baadaye Jamali walikubali kumshirikisha Nameless kama Mwandishi wa "maisha" kwenye albamu yao ya "Yours Fatally"

Yeye alikuwa miongoni mwa orodha ya watu mia moja (100) wenya ushawishi mkubwa sana nchini Kenya kama iliyotolewa na gazeti la The Standard Agosti 2007 [1][2]

Remove ads

Tuzo

  • Kisima Music Awards 2004 - Mwanamziki wa Boomba Bora
  • Kisima Music Awards 2006 - Mwanamziki Mwanaume Bora kwenya Afro Fusion & Video Bora (Sinzia) [3]
  • 2006 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) - Mwanaume Bora (Kenya) [4]
  • 2007 Tanzania Music Awards (Kilimanjaro Music Awards) - Wimbo Bora Afrika Mashariki (Sinzia) [5]
  • 2007 Channel O Music Video Awards - Mwanaume Bora( "Sinzia") [6]
  • 2008 Pearl of Africa Music Awards - Mwanaume mwanamziki Bora Kenya [7]
  • Kisima Music Awards 2008 - Mwanamzikin Mwanaume wa Mwaka & Video Bora ( "Salari") [8]
  • Tanzania Music Awards 2009 - Wimbo Bora Afrika Mashariki ( "Salari") [9]
  • 2009 MTV Africa Music Awards - Msanii wa Mwaka, Chaguo la Wasikilizaji [10]

Kuchaguliwa

  • Tanzania Music Awards 2005 - Albamu Bora Afrika Mashariki ( "On Fire") [11]
  • 2006 MTV Europe Music Awards 2006 - Mwanamziki Bora Afrika
  • 2009 MTV Africa Music Awards - Mwanamziki Bora [12]
Remove ads

Marejeo

Viunganish vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads