Ndegejinga

Familia wa ndege wakubwa wa bahari From Wikipedia, the free encyclopedia

Ndegejinga
Remove ads
Remove ads

Ndegejinga ni ndege wakubwa wa bahari wa familia Sulidae. Wana domo refu na mabawa marefu yaliyochongoka. Takriban spishi zote wana mwili mweupe na viasi mbalimbali vya nyeusi kwa mabawa na mkia. Spishi kadhaa zina namna kahawia na ndegejinga tumbo-jeupe ana rangi ya kahawa nzito na tumbo jeupe. Ndege hawa hupiga mbizi kutoka urefu mkubwa ili kukamata samaki au ngisi. Huzaa ndani ya makoloni makubwa. Jike hutaga yai moja au mayai mawili, lakini kinda atokaye kwanza katika yai lake amsukuma ndugu wake mdogo nje ya tundu. Huyu afa kwa njaa au aliwa na ndege wa aina nyingine.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Spishi za kabla ya historia

  • Sula humeralis (kati ya Pliocene)
  • Sula sulita (Peru, mwisho wa Miocene)
  • Sula magna (Peru, mwisho wa Miocene/mwanzo wa Pliocene)

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads