Hifadhi ya Ngorongoro

From Wikipedia, the free encyclopedia

Hifadhi ya Ngorongoro
Remove ads

Hifadhi ya Ngorongoro (kwa Kiingereza: "Ngorongoro Conservation Area") ni hifadhi ya taifa kaskazini mwa Tanzania inayojulikana kote duniani, hasa baada ya kuorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia.

Thumb
Makundi ya wanyamapori katika kasoko.
Thumb
Ramani ya eneo.
Thumb
Eneo la Ngorongoro lipo kaskazini mwa Tanzania.
Thumb
Ndani ya kasoko.

Kiini chake ni eneo la kasoko kubwa lenye umbali wa takriban kilomita 180 kutoka Arusha.

Kuna jumla ya wanyamapori wakubwa takriban 25,000, wakiwa pamoja na vifaru, viboko, nyumbu, pundamilia, nyati, simba, fisi na chui.

Bidii kubwa zaidi ya kulinda wanyama aina ya vifaru zinahitajika haraka kwa sababu idadi ya wanyama hao inazidi kupungua.

Mabaki ya zamadamu katika Olduvai Gorge yanaonyesha kwamba wanyama hao waliokoma walikuweko tangu miaka milioni 3 iliyopita.

Hifandhi ya ngorongoro ina mchanga unaotembea.Mchanga huo hutembea kwa kusukumwa na upepo huku ukiwa umejikusanya pamoja bila kuacha mabaki nyuma kiasi kwamba mtu mgeni hawezi kujua ulipokuwa kipindi kilichopita hadi aelezwe na wenyeji.

Mwaka 1979 Ngorongoro ilipokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO upande wa uasilia.

Katika sekta ya utalii, ambayo nchi kama nchi huitegemea kwa kiasi fulani, ni muhimu serikali iandae miundombinu, hasa barabara zenye ubora wa hali ya juu, ili zitumike kwa muda mrefu na kuboresha sekta nyingine.

Remove ads

Picha

Thumb
Kwa sababu ya aina mbalimbali za wanyama walioko, kasoko ya Ngorongoro inafahamika kama kivutio cha utalii duniani.
Thumb
Mandhari ya kasoko ya Ngorongoro.


Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads