Nikeli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nikeli ni dutu sahili ya metali na elementi. Namba atomia yake ni 28 katika mfumo radidia, uzani atomia ni 58.6934. Katika mazingira ya kawaida ni metali ngumu yenye rangi nyeupe. Alama yake ni Ni.

Nikeli huyeyuka kwa 1728 K (1455 °C) na kuchemka kwa 3186 K (2913 °C).
Inaonyesha uchumasumaku kama chuma. Haijibutiki rahisi na oksijeni, hivyo inatumiwa sana pamoja na chuma au metali kwa mchanganyiko au kama ganda la nje kwa kusidi la kuzuia kutu.
Ina hatari kwa afya ya binadamu. Watu wasio wachache hupata mziro wakigusa nikeli mara kwa mara. Kwa sababu hiyo vifaa vya kiganga vilivyokuwa vya nikeli siku hizi vinatengenezwa ama na nikeli kidogo au bila.
Kiasi cha miligramu 50 kinatosha kumdhuru au hata kumwua mtu.
Nikeli iligunduliwa mwaka wa 1751, lakini, muda mrefu kabla ya hapo, wachimbaji wa Saxon walijua vizuri madini hayo, ambayo yalionekana kama shaba na ilitumika katika utengenezaji wa glasi kwa uchoraji glasi kijani.
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads