Nikodemo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Nikodemo
Remove ads

Nikodemo (kwa Kigiriki Νικόδημος, Nikodemos) alikuwa mwalimu wa Torati wa madhehebu ya Mafarisayo tena mwanabaraza wa Baraza la Israeli katika karne ya 1 BK.

Thumb
Nikodemo akisaidia kushusha maiti ya Yesu kutoka msalabani (Pietà, sanamu iliyochongwa na Michelangelo).

Anaheshimiwa na Wakristo wengi kama mtakatifu, ingawa sikukuu yake inaadhimishwa katika tarehe tofautitofauti, hasa tarehe 31 Agosti[1].

Remove ads

Nikodemo katika Injili

Anajulikana kwa sababu ya kutajwa mara kadhaa katika Injili ya Yohane,[2] kama mtu aliyevutiwa na Yesu Kristo ingawa aliogopa maneno ya Wayahudi wenzake.

Ndiyo sababu alimtembelea usiku ili kumuuliza maswali ya dini yao bila kujulikana (Yoh 3:1–21).

Baadaye katika baraza alimtetea Yesu kwamba si haki kuhukumu mtu bila kumsikiliza kwanza, lakini alinyamazishwa (Yoh 7:50–51).

Hatimaye alimsaidia Yosefu wa Arimataya, ambaye alitarajia Ufalme wa Mungu uliotangazwa na Yesu, akachukua jukumu la kumzika (Yoh 19:39–42) [3].

Remove ads

Nikodemo katika picha

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads