Niseforo wa Konstantinopoli

From Wikipedia, the free encyclopedia

Niseforo wa Konstantinopoli
Remove ads

Niseforo I wa Konstantinopoli (kwa Kigiriki: Νικηφόρος Α΄, Nikēphoros I; Konstantinopoli, leo Istanbul nchini Uturuki, 758 hivi Konstantinopoli, 5 Aprili 828) alikuwa mwandishi wa Kikristo wa Dola la Bizanti na Patriarki wa Konstantinopoli tangu 12 Aprili 806 hadi 13 Machi 815.[1][2]

Thumb
Mchoro mdogo wa Nikephoros I akipita juu ya Yohane VII wa Konstantinopoli.

Aliondolewa madarakani na kaisari Leo V na kupelekwa kuishi monasterini kwa sababu ya kutetea matumizi ya picha takatifu [3].

Huko aliishi muda mrefu akiendelea kuandika ili kutetea matumizi hayo[4].

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Machi au 2 Juni[5].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads