Nkem Owoh
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nkem Owoh ni muigizaji na mchekeshaji wa Nigeria. Mwaka 2008 alishinda tuzo ya African Movie Academy Award kama Muigizaji Bora katika sehemu ya uongozi. [1]
Maisha Yake ya Utotoni
Owoh alizaliwa Enugu Nigeria Baada ya masomo yake ya msingi na ya upili, alienda Chuo Kikuu cha Ilorin alikosomea uhandisi. Kama bado anasoma masomo ya chuo kikuu, Owoh alianza uigizaji katika televisheni na filamu.
Kazi
Owoh alikuwa kati ya waigizaji wakuu katika filamu ya 2003 ya Osuofia i London . Anajulikana pia kwa kuuimba wimbo wa I Go Chop Your Dollar, unaohusu ufisadi wa ada ya mapema. Wimbo huu ulitumika katika filamu ya The Master ambapo Owoh hucheza kama mtapeli.[2] Tume ya Uhalifu wa Fedha na Uchumi na Tume ya Utangazaji ya Nigeria ilipiga marufuku wimbo huo[3]. Mwaka 2007 alikamatwa na polisi mjini Amsterdam, Uholanzi(kitongoji Bijlmermeer katika eneo la Amsterdam Zuidoost) kama matokeo ya uchunguzi wa miezi 7 ulioitwa "Operation Apollo".[2] Owoh alikuwa akitumbuiza wakati polisi walivamia pahali pale na kuwatia mbaroni watu 111 kwa tuhuma za udanganyifu makosa ya uhamiaji. Owoh baadaye aliachiliwa huru.[3][4][5] Mwezi Novemba 2009, Owoh alitekwa nyara eneo la mashariki mwa Nigera. Wateka nyara walitaka naira milioni 15 kama makombozi. Aliachiliwa huru baada ya familia yake kutoa naira milioni 1.4 kama makombozi.
Remove ads
Filamu
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads