Watrapisti
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Watrapisti (ufupisho wa jina la shirika lao ni OCSO, Ordo Cistercensium Strictae Observantiae) ni wamonaki wa Kanisa Katoliki wanaofuata kikamilifu urekebisho wa umonaki wa Kibenedikto ambao ulianza Citeaux (leo nchini Ufaransa) tarehe 21 Machi 1098 ukaenea haraka kila mahali katika karne ya 12, hasa kutokana na mvuto wa mwanashirika Bernardo wa Clairvaux.
Jina linatokana na monasteri ya La Trappe, Normandy, ambapo mwaka 1664 Armand Jean le Bouthillier de Rancé alianzisha tapo lenye msimamo mkali zaidi kuhusu kazi za mikono, kimya, kujinyima chakula, kujitenga na ulimwengu na kukataa masomo mengi.
Mwishoni mwa mwaka 2020) walikuwa 1,608 (mapadri 500 hivi) kwenye monasteri 87 katika mabara yote [1].
Wasitoo wengine wote wanaunda shirikisho la O.Cist..
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads