Bata mkia-ngumu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bata mkia-ngumu
Remove ads

Mabata mkia-ngumu ni ndege wa maji wa nusufamilia Oxyurinae katika familia Anatidae. Manyoya ya mkia wao ni makavu na yametandawaa mara nyingi. Rangi ya dume ni kahawia au kahawiachekundu na domo lake lililovimba msingini ni buluu; jike ni mweusi au kijivu wenye domo la rangi ile ile. Spishi hizi huzamia kabisa ili kutafuta chakula. Hula mimea na invertebrata ya maji. Miguu yao iko nyuma sana, kama ile ya mabata wazamaji, ili kujisogeza mbele vizuri ndani ya maji. Kwa sababu hiyo hawawezi kutembea vizuri. Hujenga tago lao ndani ya uoto mzito wa maji. Jike huyataga mayai 3-8, lakini pengine hadi mayai 12 yanapatikana kwa sababu jike mwingine ameongezea mayai yake.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Spishi ya kabla ya historia

  • Biziura delautouri (De Lautour's or New Zealand Musk Duck, Holocene ya New Zealand)
  • Tirarinetta kanunka (Piocene ya Australia Kusi)

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads