Kisaidizi binafsi cha kidijitali
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kisaidizi binafsi cha kidijitali (Kiingereza: Personal digital assistant; kifupi PDA) ni kifaa kidogo cha mkononi chenye matumizi mengi, ambacho hutumika kusaidia kupanga taarifa binafsi. Baada ya kuwa maarufu sana miaka ya 1990 na 2000, PDA nyingi zilianza kupoteza umaarufu baada ya watu wengi kuanza kutumia simujaja zenye uwezo mkubwa zaidi, hasa zile zinazotumia iOS na Android mwishoni mwa miaka ya 2000, na kwa hiyo matumizi yake yakapungua kwa haraka.[1][2]

PDA huwa na skrini ya kuonyesha vitu kwa njia ya kielektroniki. Aina nyingi pia huwa na uwezo wa kutoa sauti, hivyo zinaweza kutumika kama kicheza media kidogo (kifaa cha kubeba na kucheza sauti/video), na zingine pia kama simu. Kufikia mwanzo wa miaka ya 2000, karibu kila PDA ilikuwa na uwezo wa kuunganishwa na Internet, intranets au extranets kwa kutumia Wi-Fi au WAN, zisizo na waya. Pia nyingi zikawa na kivinjari cha simu. Baadhi ya PDA za baadaye zilitumia kioo cha kupapasa badala ya vitufe.
Remove ads
Historia

PDA ya kwanza kabisa iliitwa Organiser, na ilitolewa mwaka 1984 na kampuni ya Psion. Kisha ikafuata Psion Series 3 mwaka 1991, ambayo ilianza kufanana na PDA tunazozifahamu, ikiwa na kibodi kamili.[3][4] Neno PDA lilitumiwa kwa mara ya kwanza tarehe 7 Januari 1992 na Mkurugenzi Mkuu wa Apple Inc., John Sculley, katika maonesho ya Consumer Electronics Show huko Las Vegas, Nevada, akimaanisha Apple Newton.[5]

Mwaka 1994, IBM ilitoa PDA ya kwanza yenye uwezo wa kutumia simu ya analojia, iitwayo IBM Simon, ambayo pia inaweza kuchukuliwa kama simujanja ya kwanza. Kisha mwaka 1996, Nokia ilitoa PDA yenye simu ya kidigitali, iitwayo 9000 Communicator.
Kampuni nyingine iliyokuwa ya kwanza katika soko hili ni Palm, ambayo ilianza kuuza mfululizo wa bidhaa za PDA mwezi Machi 1996.[6] Palm ilikuja kutawala soko la PDAs hadi zilipoanza kushindanishwa na vifaa vya Pocket PC mwanzoni mwa miaka ya 2000.[7]
Kufikia katikati ya miaka ya 2000, karibu kila PDA ilianza kuwa simujanja, kwa kuwa zile ambazo hazikuwa na uwezo wa kupiga simu zilianza kupotea sokoni.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads