Android
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Android ni jina la aina ya mfumo huria wa uendeshaji wa simu za mikononi. Mfumo huo hutumiwa hasa katika simujanja, kama vile Google inavyomiliki Google Nexus, vilevile kampuni nyingine zinafanya vivyohivyo ikiwa ni pamoja na HTC na Samsung. Mfumo huo wa uendeshaji umepata kutumika pia katika kompyuta bapa kama vile Motorola, Xoom na Amazon Kindle Fire.[1]

Google imetoa pia Android nyingine kama vile Android TV ya televisheni, Android Auto ya magari, Android Things kwa ajili ya vifaajanja na Wear OS ya saa ya mkononi. Aina nyingine za Android hutumiwa pia kwa michezo ya kompyuta na kamera za kidijiti.
Android mwanzoni iliundwa na Android Inc. kabla ya kununuliwa na Google mwaka 2005. Matumizi rasmi ya kibiashara yalianza mnamo Septemba 2008. Toka mwaka huo Android imetoa matoleo mbalimbali. Toleo la sasa ni 9 "Pie" lililotolewa Agosti 2018. Android Q beta ilitolewa Machi 13, 2019. Programu ya msingi ya Android inaitwa Android Open Source Project (AOSP) ambayo hutolewa kwa Leseni ya Apache.
Google inasema zaidi ya simujanja milioni 1.3 zenye mfumo wa Android zinauzwa kila siku.[2] Hii imeifanya Android kuwa miongoni mwa mifumo ya uendeshaji wa simu inayotumika sana duniani.
Remove ads
Programu za Android
Programu za Android, zinaitwa "apps" za simu za mkononi, ambazo zinatoka duka la Google Play. Programu hizi zinatumia mtindo wa *.apk faili. Programu za Android zimetengenezwa na lugha ya Python, C, C++, au lugha za Java lakini Kusano za mtumiaji daima hutengenezwa kwa kutumia Java na XML. Kuna apps zaidi ya milioni 2.8 zinapatikana katika Android.[3]
Kati ya programu hizi kuna apps za manufaa kama vile za kusaidia utendaji kazi wa simu kwa mfano app ya kusaidia utendaji kazi wa simu mtu akicheza michezo ya simu[4], burudani kama vile muziki na michezo ya simu na apps za kulaghai watumiaji au za kutumia kufanya ulaghai kama vile apps za kufichua nenosiri au kuiba mtandao wa intaneti. Ni muhimu mtu kuwa na uhakika na apps anazoziweka kwa simu yake.
Remove ads
Matoleo ya Android na majina yake
Samsung Galaxy yenye toleo la Android
Kila toleo la bidhaa la Android lina namba na jina linatokana na majina ya vitu vitamutamu. Namba za matoleo na majina yake ni:
- Matoleo ya Beta: Ni Astro na Bender
- 1.5: Cupcake
- 1.6: Donut
- 2.0 and 2.1: Eclair
- 2.2: Froyo (Frozen Yogurt)
- 2.3: Gingerbread
- 3.x: Honeycomb (a tablet-only version)
- 4.0: Ice Cream Sandwich
- 4.1, 4.2 and 4.3: Jelly Bean
- 4.4: KitKat
- 5.0 and 5.1: Lollipop
- 6.0 and 6.0.1: Marshmallow[5]
- 7.0 and 7.1: Nougat
- 8.0 and 8.1: Oreo[6]
- 9.0: Pie
- 10: Quince Tart
- 11: Red Velvet Cake
- 12: Snow Cone
- 13: Tiramisu
- 14: Upside Down Cake
- 15: Vanilla Ice Cream
- Coloring Boook For Kids for Android[7]
Remove ads
Kileta bahati

Kileta bahati cha Android ni cha rangi ya kijani. Ingawa hakina jina maalum, inaaminika kuwa wafanyakazi wa Android hukiita "Bugdroid".[8]
Kilibuniwa na aliyekuwa mbunifu wa Google Irina Blok Novemba 5, 2007.
Tazama pia
- Mfumo wa uendeshaji
- Linux
- Google Nexus
- Google Pixel
- Samsung Galaxy
- Androidland
- iOS
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads