Pai

From Wikipedia, the free encyclopedia

Pai
Remove ads
Remove ads

Pai (jina la herufi ya Kigiriki π) ni namba ya duara kwa maana ya uwiano wa urefu wa mzingo na ule wa kipenyo.

Thumb
Duara yenye kipenyo cha 1 ina mzingo mwenye urefu wa π
Thumb
Uwiano wa urefu wa mzingo na ule wa kipenyo ni 3 na kitu. Uwiano kamili unaitwa π, pai.

Jinsi ilivyo kawaida kwa herufi mbalimbali za Kigiriki, pai pia inatumika kama kifupisho kwa ajili ya maarifa na dhana za hesabu na fisikia.

Imejulikana hasa kama namba ya duara. Ikiandikwa inanaza 3.141592653589793238462643... lakini haiwezi kuandikwa kamili kwa kuongeza tarakimu baada ya nukta maana hakuna mwisho. Namba za aina hii zisizo sehemu ya namba nyingine au ambazo haziwezi kuonyeshwa kuwa wianisho safi baina namba kamili huitwa namba zisizowiana.

Chamkano cha 22/7 ni karibu zaidi na pai na 355/113 ni karibu zaidi tena.

Wanahisabati duniani husheherekea sikukuu ya pai tarehe 14 Machi au pia 22 Julai.

Remove ads

Marejeo

Loading content...

Viungo vya nje

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads