Papia wa Hierapoli

Baba wa Kitume wa Ugiriki, Askofu wa Hierapolis na mwandishi (c.60-c.130 AD) From Wikipedia, the free encyclopedia

Papia wa Hierapoli
Remove ads

Papia wa Hierapoli (70 hivi - 155 hivi) alikuwa mfuasi wa Mtume Yohane pamoja na Polikarpo.

Thumb
Papias

Baadaye akawa askofu au kiongozi wa ushirika wa Kikristo mjini Hierapoli (karibu na Pamukkale ya leo katika Uturuki)[1].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Februari[2].

Maandishi

Papia ni maarufu katika historia ya Ukristo kwa sababu ni mtu wa kwanza anayejulikana kukusanya habari juu ya waandishi wa Agano Jipya. Aliandika habari hizo katika vitabu vitano vilivyoitwa "Maelezo kuhusu maneno ya Bwana (Yesu)".

Maandiko hayo yamepotea lakini sehemu za yaliyomo yake zimehifadhiwa katika vitabu vingine vya Irenaeus wa Lyons ("Dhidi ya uzushi") na Eusebi wa Kaisarea ambao walikuwa na vitabu vyake wakati wa kuandika vya kwao.

Papia alimtaja Mtume Mathayo kama mwandishi wa Injili ya Mathayo na "Presbiteri Marko mfasiri wa Petro" kama mwandishi wa Injili ya Marko.

Waandishi wa baadaye katika Ukristo wa kale hawakukubaliana juu yake. Wengine walimsifu, wengine walimwona kama mtu asiye na habari za maana.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads