Mtakatifu Marko
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Mtakatifu Marko (kwa Kilatini Mārcus; kwa Kigiriki Μᾶρκος; aliishi katika karne ya 1 BK) alikuwa Myahudi wa Yerusalemu aliyeongokea mapema Ukristo pamoja na Maria mama yake. Kanisa la kwanza lilikuwa linakusanyika nyumbani mwao.

Alifanya kazi na mitume Paulo na Barnaba katika kuhubiri Injili huko Kupro na Uturuki wa leo.
Baadaye alikuwa na Mtume Petro na Paulo katika mji wa Roma hadi walipouawa na serikali ya Kaisari Nero (dhuluma ya miaka 64-68).
Ndipo, kwa kufuata mafundisho ya Petro aliyemwita mwanae, alipoamua kuandika Injili ya kwanza, iliyotumiwa na kufuatwa na Mtume Mathayo na Mwinjili Luka, ingawa katika orodha za Biblia inashika nafasi ya pili.
Kadiri ya mapokeo alifariki wakati akifanya kazi ya kuanzisha Kanisa huko Aleksandria nchini Misri [1].
Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads