Paul Kagame
Mwanasiasa kutoka Rwanda From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Paul Kagame (amezaliwa 23 Oktoba 1957) ni Rais aliyepo madarakani nchini Rwanda.
Remove ads
Ijapokuwa ni mmoja kati ya mwanajumuiya ya Watusi, ameonekana kuuanganisha Utusi wake. Huyu ndiye mhusika mkuu wa kuondosha Uhutu na Utusi na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo (Mauaji ya kimbari ya Rwanda).
Hata hivyo, mara nyingi anatazamwa kama dikteta kwa kuwa na rekodi mbaya ya ukiukaji wa haki za binadamu.
Kagame ameweka kipaumbele katika maendeleo ya taifa, akilenga kufanya Rwanda isiwe tena kati ya nchi maskini kufikia mwaka 2020. Kweli nchi imepiga hatua kubwa katika masuala mengi, kama vile afya, teknolojia na elimu. Kati ya miaka 2004 na 2010 pato liliongezeka 8% kwa mwaka.
Uhusiano na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo si mzuri, hata baada ya vita kusimamishwa rasmi mwaka 2003; asasi za kutetea haki za binadamu zinadai Rwanda inaendelea kutegemeza makundi ya waasi ili kufaidika na maliasili ya nchi hiyo jirani, ingawa Kagame anakanusha.
Remove ads
Viungo vya nje
- Official website
- Paul Kagame at the Internet Movie Database
- Shughuli au kuhusu Paul Kagame katika maktaba ya WorldCat catalog
![]() |
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Paul Kagame kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads