Paulino wa Nola
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Paulino wa Nola (jina kamili kwa Kilatini: Pontius Meropius Anicius Paulinus; Bordeaux, leo nchini Ufaransa, takriban 355 – Nola, karibu na Napoli, Italia, 22 Juni 431) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki huko Nola.

Tangu kale ametambuliwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kuwa mtakatifu.
Maisha
Paulino wa Nola alikuwa mwanasiasa maarufu tena tajiri, akaoa na kupata mtoto wa kiume.
Lakini alitamani kuishi maisha maadilifu, na hivi akabatizwa, akaachana na mali yake yote, akaanza kuishi kimonaki huko Nola, leo katika mkoa wa Campania nchini Italia, kuanzia mwaka wa 393.
Aliteuliwa kuwa askofu wa Nola, ambako alikuza sana heshima kwa Felisi wa Nola, na kuwasaidia waliokwenda huko kuhiji.
Vilevile alijitahidi kupunguza taabu za watu wa wakati huo.
Aliandikiana barua na watu wengi maarufu, kama vile Agostino wa Hippo, akatunga mashairi kadhaa yenye ufasaha wa hali ya juu sana[2].
Remove ads
Tazama pia
Maandishi
- Ausonius, & Paulinus of Nola, Ausone et Paulin de Nole correspondance, tr. D. Amherdt (2004) [Latin text; French tr.]
- Paulinus of Nola, Sancti Pontii Meropii Paulini Nolani Opera, ed. G. de Hartel (2nd. ed. cur. M. Kamptner, 2 vols., 1999) [v.1. Epistulae; v.2. Carmina. Latin texts]
- Paulinus of Nola, Paolino di Nola I Carmi ..., ed. A. Ruggiero (1996)
- Paulinus of Nola, Paolino di Nola Le Lettere. Testo latino con introduzione, traduzione italiana ..., ed. G. Santaniello (2 vols., 1992)
- Paulinus of Nola, The Poems of Paulinus of Nola translated ... by P. G. Walsh (1975)
- Paulinus of Nola, Letters of St Paulinus of Nola translated ... by P. G. Walsh (2 vols., 1966-7)
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads