Paulo Miki
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Paulo Miki (Kyoto, takriban 1565 – Nagasaki, 5 Februari 1597) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki nchini Japani.

Ametambuliwa kuwa mtakatifu kama mfiadini.
Sikukuu yake ni tarehe 6 Februari[1].
Maisha
Paulo Miki alizaliwa nchini Japani kati ya miaka 1564 na 1566.
Alijiunga na Shirika la Yesu (Wajesuiti), akahubiri Injili kwa ufanisi [2].
Lakini dhuluma dhidi ya Wakatoliki zilipozidi, yeye na wenzake 25 (mapadri na watawa 8 na walei 17[3]) walikamatwa, walitukanwa na kuteswa vikali, na hatimaye wakasulubiwa huko Nagasaki tarehe 5 Februari mwaka 1597, huku wakifurahia neema ya kuuawa namna ileile ya Yesu [4].
Hadi sasa Wafiadini wa Japani waliotangazwa watakatifu ni 42, mbali na wenye heri 393.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads