Paulo wa Tebe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Paulo wa Tebe (230 hivi - Jangwa la Thebe, 5 Januari 342) anakumbukwa kama mkaapweke wa Kikristo wa kwanza nchini Misri.




Anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi tangu zamani sana kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 10 Januari[1] au 15 Januari[2].
Remove ads
Maisha
Chanzo cha habari kuhusu maisha yake ni kitabu cha Jeromu, Vita Sanctii Pauli primi eremitae, kilichoandikwa katika nusu ya pili ya karne IV.
Wakati wa dhuluma ya Kaisari Decius, Paulo, kijana msomi na tajiri wa Misri, alilazimika kukimbia mji wake na kwenda jangwani kisha kushtakiwa na jamaa zake (waliotamani kujipatia mali yake) kuwa ni Mkristo.
Baada ya dhuluma hiyo kali kwisha mapema, Paulo hakurudi nyuma, bali aliendelea kuishi upwekeni hadi kifo chake.
Alipokaribia kufa alitembelewa na Antoni Abati, akamuomba amzike amefunikwa joho alilopewa na Atanasi wa Aleksandria.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Vyanzo kwa Kiswahili
Vyanzo kwa lugha nyingine
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads