Petro Apselamo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Petro Apselamo (pia: Petrus Abselamus, Petrus Absalon, Petrus Balsamus na Petro wa Atroa; Anea, karibu na Eleutheropolis, leo nchini Israeli, karne ya 3 - Kaisarea Baharini, Israeli, 11 Januari 309[1][2]) alikuwa Mkristo aliyefia imani yake kwa kuchomwa moto wakati wa dhuluma ya kaisari Masimino baada ya kukataa mashauri mengi ya kumtaka aokoe ujana wake[3].
Alijulikana kwa nguvu yake kubwa,[4] lakini pia kwa huruma na moyo wa ibada [5].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Januari [6][7] au 14 Oktoba. [8].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads