Petro Hong Pyongju

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Petro Hong Pyongju (alifariki Dangkogae, 31 Januari 1840) ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 17911888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.

Yeye na wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[1]

Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba, lakini ya kwake na ya wenzake watano (Augustino Pak Chongwon, Maria Yi Indok, Magdalena Son So-byg, Agata Yi Kyng-i, Agata Kwn Chin-i) ni tarehe 31 Januari, ambapo yeye na hao, baada ya kuteswa sana, walizidi kukiri imani yao hadi walipokatwa vichwa[2][3].

Remove ads

Mazingira

Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[4] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[5].

Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads