Phalangopsidae
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Phalangopsidae ni familia ya wadudu wanaofanana na nyenje-ardhi (Gryllidae). Nchini Afrika Kusini huitwa “bell crickets” au nyenje kengele. Inapendekezwa kutumia jina hili angalau kwa spishi za Afrika.
Makala hii inahitaji vyanzo zaidi ili kuwezesha kuonyesha uthibitisho. |
Hii ni moja ya familia kubwa zaidi za nyenje yenye spishi zinazotofautiana sana. Kwa hivyo ni ngumu kutoa maelezo ya jumla ya mofolojia na tabia zao. Spishi nyingi huonekana kuishi katika misitu, huku idadi nzuri zikiishi katika mapango. Wadudu hao hukiakia wakati wa usiku na hula dutu za kioganiki kati ya takataka za majani au takataka nyingine katika kisa cha mapango. Wakati wa mchana hujificha kwenye mashimo. Spishi nyingi hupendelea hali ya unyevunyevu, ingawa spishi nyingine huko Australia na visiwa kadhaa vya Pasifiki huishi katika hali kavu[1].
Remove ads
Spishi za Afrika ya Mashariki
- Homoeogryllus xanthographus
- Paragryllodes affinis
- Paragryllodes amani
- Paragryllodes borgerti
- Paragryllodes campanella
- Paragryllodes dissimilis
- Paragryllodes kenyanus
- Paragryllodes minor
- Paragryllodes pyrrhopterus
- Paragryllodes silvaepluvialis
- Paragryllodes unicolor
Picha
- Nyenje kengele kusi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads