Philemon Ndesamburo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Philemon Kiwelu Ndesamburo (alifahamika kama ‘Mzee Ndesamburo’; 19 Februari 1935 - 31 Mei 2017) alikuwa mbunge wa jimbo la Moshi Mjini katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.[1] Alipata nafasi ya kuwa mbunge kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mwanasiasa huyo aliingia katika kinyang’anyiro hicho na kufanikiwa kuwa mbunge tangu mwaka 2000.
Alifariki dunia katika hospitali ya rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi alikokuwa akipatiwa matibabu. Taarifa za kifo chake zilithibitishwa na Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro Basil Lema. Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Fredrick Shoo aliongoza ibada ya mazishi ya mwanasiasa mkongwe iliyofanyika katika Kanisa la Lutheran Kiboroloni.
Katika mahubiri kwenye ibada hiyo Askofu Shoo alisema kifo cha Ndesamburo kimeacha pengo kubwa kwa familia na taifa la Tanzania kutokana na mchango wake wa pekee. “Mzee Ndesamaburo alikuwa mzalendo wa Tanzania ambaye hakumbagua mtu yeyote bila kujali dini yake, kabila au chama cha siasa. Zaidi ya yote, Mzee Ndesamburo alikuwa mtu mwenye hofu ya Mungu,” alisema Askofu Shoo Jumatano ya Juni 7, 2017.
Remove ads
Tazama pia
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads