Ponsyo Pilato
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Ponsyo Pilato (kwa Kilatini Pontius Pilatus; kwa Kigiriki Πόντιος Πιλᾶτος; kwa Kiebrania פונטיוס פילאטוס; alikuwa liwali wa kiroma katika Palestina kwenye miaka 26-36.

Anajulikana kutoka vyanzo mbalimbali, lakini hasa kwa sababu ya Injili kumtaja kama hakimu aliyempeleka Yesu kuuawa msalabani. Vyanzo vingine ni katika maandiko ya Yosefu Flavius, Tacitus na Filo wa Aleksandria.
Waandishi Wayahudi Josephus na Philo wanamwonyesha kama mtawala mkali asiyeheshimu utamaduni na imani ya wenyeji wa Palestina. Baada ya kutumia unyama katika ukandamizaji wa Wasamaria aliitwa kurudi Roma na kufika mbele ya Kaisari. Hakuna habari za uhakika kuhusu maisha yake ya baadaye.
Kanisa la Ethiopia linafuata hadithi ya kwamba aliongoka, hivyo linamheshimu kama mtakatifu.
Kadiri ya mapokeo mengine, alijiua.
Remove ads
Tazama pia
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
![]() |
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ponsyo Pilato kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads