Pinocchio (filamu ya 1940)

filamu ya katuni ya Kimarekani ya mwaka wa 1940 iliyotayarishwa na Walt Disney From Wikipedia, the free encyclopedia

Pinocchio (filamu ya 1940)
Remove ads

Pinocchio ni filamu ya katuni ya Marekani ya mwaka wa 1940 iliyotayarishwa na Walt Disney na inatokana na hadithi ya Kiitalia ya Carlo Collodi aliyesimulia vituko vya mwanaserere Pinokyo (Le avventure di Pinocchio). Kitabu hicho kiliwahi kutafsiriwa na Tanganyika Mission Press kwa Kiswahili mwaka 1965 na kuwa maarufu Afrika Mashariki kwa jina Mambo yalioyompata Pinokyo.

Ukweli wa haraka Imeongozwa na, Imetayarishwa na ...

Hii ni filamu ya pili kutolewa katika mfululizo wa filamu za katuni za Walt Disney, na ilitengenezwa baada ya kupata mafanikio makubwa katika filamu ya awali ya Snow White and the Seven Dwarfs na ilitolewa katika makumbi na RKO Radio Pictures tarehe 7 Februari 1940.

Hadithi ya filamu hii inamhusisha kikaragosi cha mbao anayeitwa Pinocchio (sauti ya Dickie Jones) ameletwa maishani na kichimbakazi cha buluu (Evelyn Venable), ambaye anamweleza kwamba anaweza kuwa kijana wa kweli iwapo atajibitisha kama ni "jasiri, mkweli, na si mchoyo". Hivyo kikaragosi huyo anaianza safari ili ili awe kijana wa kweli, ambamo kunatokea mashambulizi mengi wakati wa safari hiyo.

Ndani yake wanakuja Aurelius Battaglia, William Cottrell, Otto Englander, Erdman Penner, Joseph Sabo, Ted Sears, na Webb Smith kutoka katika kitabu cha Collodi. Matayarisho yake yalisimamiwa na Ben Sharpsteen na Hamilton Luske, na mfululizo wa filamu uliongozwa na Norman Ferguson, Thornton Hee, Wilfred Jackson, Jack Kinney, na Bill Roberts.

Remove ads

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads