Mwogeleaji-juuchini kibete
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Waogeleaji-juuchini vibete ni wadudu wadogo sana wa maji wa familia Helotrephidae na Pleidae katika oda ya chini Nepomorpha ya oda Hemiptera wanaoogelea mgongo ukiwa chini. Pleidaei ina spishi 41, ambazo 3 zinatokea katika Afrika, na Helotrephidae ina spishi nyingi, nyingi sana katika Asia ya Kusini na Kusini-mashariki na 23 katika Afrika. Wadudu hawa ni mbuai.
Remove ads
Maelezo
Wadudu hawa wana ukubwa wa mm 1.5-3.5[1][2]. Mwili wao una umbo la duaradufu na mgongo wa mbenuko wa juu, unaofanana na mbawakawa wadogo sana. Miguu ya nyuma si mirefu sana, haina nywele na haifai sana kuogelea, ikitumiwa zaidi kwa kusota kati ya mimea ya maji. Spishi kadhaa zina mabawa yaliyopunguka na kwa hivyo haziwezi kuruka. Walakini, spishi nyingi zina mabawa yaliyokua kikamilifu, lakini hata hivyo haziruki vizuri sana. Katika Helotrephidae, kichwa na pronoto zimeunganishwa[3].
Remove ads
Biolojia
Waogeleaji-juuchini vibete wakiogelea, hutumia miguu yao ya nyuma. Ingawa hiyo haina umbo kama ile ya waogeleaji-juuchini wakubwa zaidi, inafanya kazi vizuri kwa sababu ya udogo wa wadudu hawa. Hata hivyo, mara nyingi sana, hutambaa kati ya uoto wa majini au kwenye miamba iliyo chini ya maji. Ili kupumua, hukusanya hewa kutoka kwenye uso wa maji, ambayo huhifadhiwa kati ya nywele fupi kwenye upande wao wa tumbo (Pleidae) au chini ya mabawa ya mbele (Helotrephidae). Hutokea katika maji matamu tulivu yenye mimea, ingawa baadhi ya Helotrephidae huishi kwenye miamba chini ya maporomoko ya maji. Chakula chao ni gegereka wadogo, viluwiluwi wa mbu na invertebrata wengine wadogo, hata wadudu mkia-fyatuo wa maji ambao huwanyakua usoni kwa maji. Kama vile kunguni-maji wengine, huingiza mate ndani ya mbuawa wao ili kuyeyusha tishu, ambazo kisha hufyonza. Waogeleaji-juuchini vibete hawashiki mbuawa wadogo kuliko wao, kama vidudu-gurudumu, kwa sababu miguu yao mifupi ya mbele haiwezi kuwashughulikia.[4].
Remove ads
Spishi za Afrika
Helotrephidae
- Esakiella acuminata
- Esakiella buea
- Esakiella chinai
- Esakiella didyi
- Esakiella eremita
- Esakiella gereckei
- Esakiella goldenschmidti
- Esakiella hancocki
- Esakiella hungerfordi
- Esakiella hutchinsoni
- Esakiella madli
- Esakiella marlieri
- Esakiella milloti
- Esakiella mutsoriai
- Esakiella nairobi
- Esakiella nimbae
- Esakiella rivularius
- Esakiella starmuehlneri
- Esakiella wenchiana
- Idiocoris lithophilus
- Paralimnotrephes villiersi
- Paskia minutissima
- Pseudohydrotrephes moramongae
Pleidae
- Paraplea piccanina
- Paraplea pullula
- Plea minutissima
Picha
- Helotrephes indicus
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads