Pomposa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Pomposa (alizaliwa na kufariki Cordoba, Hispania, 19 Septemba 853) alikuwa mtawa bikira aliyeuawa na Waislamu waliotawala nchi hiyo.
Ili kupata heshima hiyo, alipopata taarifa ya kifodini cha Kolomba wa Cordoba, alitoroka monasteri yake akaenda kukiri imani yake kwa ushujaa mbele ya hakimu akakatwa kichwa mara moja mbele ya malango ya ikulu [1][2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Septemba[3].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads