Poto

From Wikipedia, the free encyclopedia

Poto
Remove ads

Poto au koni ni wanyama wadogo wa nusufamilia Perodicticinae katika familia Lorisidae. Wamo miongoni mwa wanyama wa asili wa jamaa ya binadamu. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara. Wanaishi mitini kwa misitu ya mvua ya Afrika ya Magharibi na ya Kati, na wanateremka chini kwa nadra. Hukiakia usiku na hulala mchana katikati ya majani. Kwa hivyo wana macho makubwa ili kuona vizuri kwa giza. Mkia ni mfupi na haupo takriban kwa spishi za Arctocebus. Manyoya yao ni mazito kama sufu yenye rangi ya kijivu, ya kahawa au ya dhahabu. Huenda polepole sana. Wana kucha kama zile za watu, isipokuwa ule wa kidole cha pili cha miguu ambao ni mrefu wenye ncha kali na hutumika kwa kusafisha manyoya. Kidole cha pili cha mikono ni karibu ya kutoweka. Hula matunda, sandarusi, wadudu na wanyama wadodo.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi

  • Arctocebus aureus, Angwantibo au Poto Dhahabu (Golden angwantibo au Golden Potto)
  • Arctocebus calabarensis, Angwantibo au Poto wa Calabar (Calabar angwantibo au Calabar Golden Potto)
  • Perodicticus potto, Koni au Poto wa Kawaida (Potto au Bosman's Potto)
  • Pseudopotto martini, Koni au Poto Rongo (False potto) – wataalamu wengi wanafikiri spishi hii ni sawa na P. potto
Remove ads

Picha

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads